-
Yehova Ni MfalmeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika. Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana.
-
-
Yehova Ni MfalmeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Kokote watakakojaribu kukimbilia watu, watakamatwa. Huenda wengine wakaponyoka msiba mmoja, lakini watanaswa katika mwingine—usalama hautakuwapo. Itakuwa kama mnyama aepukaye kuanguka shimoni, kisha anaswa mtegoni. (Linganisha Amosi 5:18, 19.) Nguvu za hukumu ya Yehova zitaachiliwa kutoka mbinguni nazo zitatikisa misingi ya nchi.
-