Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Ni Mfalme
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.”—Isaya 24:21-23.

  • Yehova Ni Mfalme
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 20. Katika nyakati za kale na leo vilevile, Yehova ‘anakuwa mfalme’ jinsi gani na lini?

      20 Basi sehemu hiyo ya unabii wa Isaya iliwaacha Wayahudi wakiwa na uhakikisho mzuri sana. Katika wakati wa Yehova ufaao, angesababisha kuanguka kwa Babiloni la kale na kuwarudisha Wayahudi nchini kwao. Mwaka wa 537 K.W.K., aonyeshapo nguvu zake na enzi yake kuu kwa niaba ya watu wake, ingeweza kusemwa kikweli kuwahusu: “Mungu wako anamiliki [“amekuwa mfalme,” NW]!” (Isaya 52:7) Leo, Yehova ‘alikuwa mfalme’ mwaka wa 1914 alipomweka Yesu Kristo kuwa Mfalme katika Ufalme Wake wa mbinguni. (Zaburi 96:10) Pia, ‘alikuwa mfalme’ mwaka wa 1919 alipoonyesha nguvu zake za kifalme kwa kuwakomboa Israeli wa kiroho kutoka utumwa wa Babiloni Mkubwa.

      21. (a) ‘Mwezi utatahayari jinsi gani, nalo jua litaonaje haya’? (b) Ni mwito gani unaosikika kote utakaokuwa na utimizo wake mkuu?

      21 Yehova ‘atakuwa mfalme’ tena amwangamizapo Babiloni Mkubwa na sehemu iliyobaki ya mfumo huu mwovu wa mambo. (Zekaria 14:9; Ufunuo 19:1, 2, 19-21) Baadaye, utawala wa Ufalme wa Yehova utakuwa mtukufu sana hivi kwamba mwezi unaomulika usiku na jua lenye kung’aa adhuhuri hazitaufikia kwa utukufu. (Linganisha Ufunuo 22:5.) Kitamathali, jua na mwezi zitaona haya kujilinganisha na utukufu wa Yehova wa majeshi. Utawala wa Yehova utakuwa mkuu kuliko zote. Wote wataziona nguvu zake na utukufu wake mkuu. (Ufunuo 4:8-11; 5:13, 14) Hilo ni tazamio zuri kama nini! Wakati huo, mwito wa Zaburi 97:1 utasikika duniani kote katika utimizo wake mkuu: “BWANA [“Yehova,” NW] ametamalaki [“amekuwa mfalme,” NW], nchi na ishangilie. Visiwa vingi na vifurahi.”

  • Yehova Ni Mfalme
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • [Picha katika ukurasa wa 269]

      Wala jua wala mwezi hazitafikia utukufu wa Yehova

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki