-
Mkono wa Yehova WainuliwaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
8, 9. (a) Ni adui gani wawili wakuu wa wanadamu watakaoondolewa? Eleza. (b) Mungu atafanya nini ili kuiondoa aibu ya watu wake?
8 Wale wanaokula sasa karamu ya kiroho ambayo Mungu ameandaa wana matazamio matukufu. Yasikilize maneno yafuatayo ya Isaya. Azilinganishapo dhambi na kifo na ‘utaji uliotandwa’ ambao husonga pumzi, au “sitara,” asema: “Katika mlima huu [Yehova] atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote.
-