-
Wokovu kwa Wanaochagua NuruMnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
-
-
“Umeliongeza Hilo Taifa”
13, 14. Watumishi watiwa-mafuta wa Yehova wamefurahia baraka gani nyingi tangu 1919?
13 Mungu alibariki mtazamo huo wa toba wa watumishi wake watiwa-mafuta katika mwaka wa 1919 na kuwapa ongezeko. Kwanza, walizingatia kukusanywa kwa washiriki wa mwisho wa Israeli wa Mungu, kisha “umati mkubwa” wa “kondoo wengine” ukaanza kukusanywa. (Ufunuo 7:9; Yohana 10:16) Baraka hizo zilitabiriwa katika unabii huu wa Isaya: “Umeliongeza hilo taifa, BWANA umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.
-
-
Wokovu kwa Wanaochagua NuruMnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
-
-
14 Leo, mipaka ya Israeli wa Mungu imepanuka na kuenea duniani pote, na umati mkubwa ambao umeongezwa sasa umefikia watu milioni sita wanaoshiriki kwa shangwe kazi ya kuhubiri habari njema. (Mathayo 24:14) Ni baraka iliyoje kutoka kwa Yehova! Hilo huleta utukufu ulioje kwa jina lake! Jina hilo husikiwa leo katika nchi 235—utimizo wa ajabu wa ahadi yake.
-