Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Endelea Kumngojea Yehova
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 5, 6. (a) Kwa nini kuungana na Misri ni kosa lenye kusababisha kifo? (b) Ni safari gani ya mapema waliyofunga watu wa Mungu ikaziayo upumbavu wa safari hii ya kwenda Misri?

      5 Isaya atoa habari zaidi, kana kwamba anajibu wazo lolote la kwamba safari hiyo ya Misri ni ya matembezi tu. “Ufunuo juu ya hayawani wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, ambayo hutoka huko simba jike na simba, nyoka na joka la moto arukaye, huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, na hazina zao juu ya nundu za ngamia.” (Isaya 30:6a) Ni wazi kwamba safari hiyo imepangwa vema. Wajumbe wapanga msafara wa ngamia na punda, wakiwapakia bidhaa zenye bei ghali na kusafiri hadi Misri kupitia nyika yenye ukiwa iliyojaa simba wanaonguruma na nyoka wenye sumu. Hatimaye, wajumbe wafika waendako na kukabidhi Wamisri hazina zao. Wanadhani kwamba sasa wamejinunulia ulinzi. Hata hivyo, Yehova asema: “Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu.

  • Endelea Kumngojea Yehova
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 6 Isaya afafanuapo safari ya wajumbe hao, huenda watu wanaomsikiliza wakakumbuka safari kama hiyo iliyofanywa siku za Musa. Baba zao wa zamani walitembea katika ‘jangwa hilo kubwa lenye kitisho.’ (Kumbukumbu la Torati 8:14-16) Ingawa hivyo, katika siku ya Musa, Waisraeli walikuwa wakisafiri kutoka Misri na kutoka utumwani. Mara hii wajumbe wanasafiri kwenda Misri na kuingia utumwani hasa. Huo ni upumbavu ulioje! Tusifanye kamwe uamuzi usio wa busara kama huo kwa kubadili uhuru wetu wa kiroho kwa utumwa!—Linganisha Wagalatia 5:1.

  • Endelea Kumngojea Yehova
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • [Picha katika ukurasa wa 305]

      Katika siku ya Musa, Waisraeli waliponyoka kutoka Misri. Katika siku ya Isaya, Yuda yaenda Misri kutafuta msaada

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki