-
Je, Utatembea Pamoja na Mungu?Mnara wa Mlinzi—2005 | Novemba 1
-
-
Tunaweza Kutembeaje Pamoja na Mungu?
9. Kwa nini nyakati nyingine Yehova alijificha kutoka kwa watu wake, lakini alitoa uhakikisho gani kwenye Isaya 30:20?
9 Tunapaswa kuzingatia kwa makini swali la tatu. Nalo ni, Tunaweza kutembeaje pamoja na Mungu? Tunapata jibu katika andiko la Isaya 30:20, 21: “Mfundishaji wako Mkuu hatajificha tena, na macho yako yatakuwa macho yanayomwona Mfundishaji Mkuu wako. Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako likisema: ‘Hii ndiyo njia.
-
-
Je, Utatembea Pamoja na Mungu?Mnara wa Mlinzi—2005 | Novemba 1
-
-
Katika masimulizi hayo yenye kutia moyo, huenda maneno ya Yehova katika mstari wa 20 yaliwakumbusha watu wake kwamba walipomwasi ni kana kwamba alijificha kutoka kwao. (Isaya 1:15; 59:2) Hata hivyo, hapa Yehova haonyeshwi akiwa amejificha bali kama ambaye amesimama mbele ya watu wake waaminifu. Huenda tukafikiria jinsi mwalimu husimama mbele ya wanafunzi wake, akiwaonyesha kile anachotaka wafanye.
-