-
Mfalme na Wakuu WakeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
17. Ni nani leo walio kama ‘binti wasiokuwa na uangalifu’ ambao Isaya anawataja?
17 Unabii wa Isaya waendelea: “Inukeni, enyi wanawake wenye raha, isikieni sauti yangu; enyi binti za watu msiokuwa na uangalifu, tegeni masikio yenu msikie matamko yangu. Maana mtataabishwa siku kadha wa kadha zaidi ya mwaka, enyi wanawake mliojikinai; kwa sababu mavuno ya mizabibu yatakoma, wakati wa kuvuna vitu vya mashamba hautakuja.
-
-
Mfalme na Wakuu WakeUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Mtazamo wa wanawake hao huenda ukatukumbusha watu wanaodai kumtumikia Mungu leo bali hawana bidii katika utumishi wake. Watu hao wamo katika “Babiloni Mkubwa, mama wa makahaba.” (Ufunuo 17:5) Kwa kielelezo, washiriki wa dini za Jumuiya ya Wakristo wanafanana sana na jinsi Isaya anavyowafafanua “wanawake” hao. Wana “raha,” pasipo kujali hukumu na fadhaiko ambazo zitawaangamiza karibuni.
-