Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Aghadhibikia Mataifa
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Siku ya Kulipa Kisasi

      9. (a) Taifa la Edomu lilitoka wapi, na kulitokea uhusiano gani baina ya Israeli na Edomu? (b) Yehova atoa agizo gani kuhusu Edomu?

      9 Sasa unabii wachagua taifa fulani ambalo lipo siku ya Isaya—Edomu. Waedomi ni wazao wa Esau (Edomu), aliyemwuzia Yakobo, ndugu yake pacha, haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mkate na chakula cha dengu. (Mwanzo 25:24-34) Esau alimchukia sana Yakobo ndugu yake kwa sababu alichukua haki ya kuwa mzaliwa wa kwanza. Baadaye mataifa ya Edomu na Israeli yakawa adui, hata ingawa yalikuwa uzao wa ndugu pacha. Kutokana na uhasama huo dhidi ya watu wa Mungu, Edomu imejiletea hasira ya kisasi ya Yehova, ambaye sasa asema: “Upanga wangu umekunywa na kushiba mbinguni; tazama, utashukia Edomu, na juu ya watu wa laana yangu, ili kuwahukumu. Upanga wa BWANA umeshiba damu, umenona kwa unono, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo waume; maana BWANA ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu.”—Isaya 34:5, 6.

      10. (a) Yehova amwangusha nani atumiapo upanga wake “mbinguni”? (b) Edomu yaonyesha mtazamo gani Yuda ishambuliwapo na Babiloni?

      10 Edomu iko katika nchi iliyoinuka, yenye milima mingi. (Yeremia 49:16; Obadia 8, 9, 19, 21) Ijapokuwa hivyo, hata ngome hizo za asili hazitafaa kitu Yehova atumiapo upanga wake wa hukumu huko “mbinguni,” akishusha watawala wa Edomu kutoka katika mahali pao palipoinuka. Edomu ina nguvu nyingi za kijeshi, na majeshi yake yashika doria katika safu ndefu za milima ili kuilinda nchi. Lakini Edomu yenye nguvu haitoi msaada wowote Yuda ishambuliwapo na majeshi ya Babiloni. Badala yake, Edomu yajawa na shangwe ionapo kuanguka kwa ufalme wa Yuda nayo yawahimiza washindi wake. (Zaburi 137:7) Edomu hata yawaandama Wayahudi wanaokimbia kuokoa uhai wao na kuwakabidhi mikononi mwa Wababiloni. (Obadia 11-14) Waedomi wapanga kutwaa nchi ya Waisraeli iliyoachwa, nao wanena kwa majivuno dhidi ya Yehova.—Ezekieli 35:10-15.

  • Yehova Aghadhibikia Mataifa
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Muda mfupi baada ya uharibifu wa Yerusalemu mwaka wa 607 K.W.K., Yehova aanza kuonyesha kisasi chake chenye haki juu ya Waedomi kupitia Nebukadreza, mfalme wa Babiloni. (Yeremia 25:15-17, 21) Majeshi ya Babiloni yavamiapo Edomu, hakuna kiwezacho kuwaokoa Waedomi!

  • Yehova Aghadhibikia Mataifa
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Wakati Ujao Usio na Matumaini kwa Jumuiya ya Wakristo

      13. Ni nani aliye kama Edomu leo, na kwa nini?

      13 Leo, kuna tengenezo ambalo mambo yake ni kama ya Edomu. Ni tengenezo gani hilo? Ni nani leo wamekuwa kwenye mstari wa mbele kutukana na kunyanyasa watumishi wa Yehova? Je, si Jumuiya ya Wakristo, kupitia jamii yake ya makasisi? Ndiyo! Jumuiya ya Wakristo imejiinua kufikia mahali pa juu kama mlima katika mambo ya ulimwengu huu. Hiyo ina cheo cha juu katika mfumo wa mambo wa wanadamu, na dini zake ni sehemu kubwa ya Babiloni Mkubwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki