-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Atalilisha kundi lake kama mchungaji, atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; na kuwachukua kifuani mwake, nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.”—Isaya 40:9-11, chapa ya 1989.
-
-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
14. (a) Isaya atoaje kielezi cha jinsi ambavyo Yehova atawaongoza watu wake kwa wororo? (b) Ni kielelezo gani kinachoonyesha jinsi ambavyo wachungaji hutunza kondoo zao kwa wororo? (Ona sanduku kwenye ukurasa wa 405.)
14 Hata hivyo, Mungu huyu mwenye nguvu ana sifa ya wororo. Isaya aeleza kwa uchangamfu jinsi Yehova atakavyowaongoza watu wake kurudi nchini kwao. Yehova ni kama mchungaji mwenye upendo anayewakusanya pamoja wana-kondoo wake na kuwabeba “kifuani” mwake. Yaonekana neno hili “kifua” larejezea mikunjo ya juu ya vazi. Nyakati nyingine wachungaji hubebea kifuani wana-kondoo waliozaliwa hivi karibuni ambao hawauwezi mwendo wa kundi. (2 Samweli 12:3) Onyesho kama hilo lenye kuvutia linalotokana na maisha ya uchungaji hapana shaka lawapa tena watu wa Yehova waliohamishwa uhakikishio wa utunzaji wake wenye upendo kwao. Kwa hakika Mungu huyo mwenye nguvu lakini mwenye wororo aweza kutumainiwa atimize yale ambayo amewaahidi!
-
-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 404, 405]
Yehova, Mchungaji Mwenye Upendo
Ili kuonyesha jinsi Yehova anavyowahangaikia watu wake, Isaya amfananisha Yehova na mchungaji anayebeba wana-kondoo wake kifuani mwake. (Isaya 40:10, 11) Yaonekana mfano huo wa Isaya ulitegemea mazoea halisi ya wachungaji wa kale. Fikiria kielelezo cha karibuni zaidi. Mtazamaji aliyewatazama wachungaji kwenye miteremko ya Mlima Hermoni katika Mashariki ya Kati asema jinsi wanavyotunza kondoo zao kwa wororo. “Kila mchungaji aliangalia kwa makini kundi lake ili kuona jinsi linavyoendelea. Akipata mwana-kondoo aliyezaliwa hivi karibuni, angemweka katika mikunjo ya . . . kanzu yake kubwa, kwa kuwa alikuwa dhaifu sana asiuweze mwendo wa mama yake. Kifua chake kilipojaa, aliwaweka wana-kondoo mabegani mwake, akiwashika kwa miguu, au kwenye mfuko au kikapu mgongoni mwa punda, hadi kondoo wachanga wauweze mwendo wa mama zao.” Je, haifariji kujua kuwa twamtumikia Mungu anayewahangaikia watu wake kwa wororo?
-
-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
16. Yehova huwaongozaje watu wake leo, na hilo huweka kiolezo gani?
16 Maneno ya Isaya 40:10, 11 yana matumizi zaidi yenye thamani kwetu leo. Inafariji kuona jinsi Yehova anavyowaongoza watu wake kwa wororo. Kama vile mchungaji aelewavyo mahitaji ya kondoo mmoja-mmoja—wakiwemo wana-kondoo wachanga wasiouweza mwendo wa wengine—ndivyo Yehova anavyouelewa udhaifu mbalimbali wa kila mmoja wa watumishi wake waaminifu. Isitoshe, Yehova aliye Mchungaji mwenye wororo huwawekea wachungaji Wakristo kiolezo. Wazee wapaswa kulitunza kundi kwa wororo, wakiiga hangaiko lenye upendo ambalo Yehova mwenyewe huonyesha. Sharti sikuzote wakumbuke maoni ya Yehova kuhusu kila mshiriki wa kundi, “ambalo alilinunua kwa damu ya Mwana wake mwenyewe.”—Matendo 20:28.
-