Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Wafarijini Watu Wangu’
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • “Ni Nani Aliyeziumba Hizi”?

      23. Sababu gani wahamishwa Wayahudi waweza kutiwa moyo, na sasa Yehova akazia jambo gani kujihusu mwenyewe?

      23 Bado kuna sababu nyingine inayowatia moyo wahamishwa Wayahudi. Yeye anayeahidi ukombozi ni Muumba wa vitu vyote na Chanzo cha nishati yenye msukumo. Ili kukazia uwezo wake wa ajabu, Yehova akazia uwezo wake unaoonekana katika uumbaji:

  • ‘Wafarijini Watu Wangu’
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake [“nishati yake yenye msukumo,” “NW”], na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.”—Isaya 40:25, 26.

  • ‘Wafarijini Watu Wangu’
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Ili kuonyesha kwamba hakuna anayelingana naye, Yehova aelekeza fikira kwenye nyota za mbinguni. Kama vile kamanda wa kijeshi anayeongoza majeshi yake, ndivyo Yehova anavyoongoza nyota. Iwapo angezikusanya, ‘hapana moja isingekuwapo mahali pake.’ Ingawa idadi ya nyota ni kubwa, yeye huziita kila moja kwa jina, kwa kutumia jina la kibinafsi au mtajo ulio kama jina. Kama vile wanajeshi watiifu, nyota hukaa mahali pake na kufuata utaratibu ufaao, kwa kuwa Kiongozi wao ana wingi wa “nishati yenye msukumo” naye ni “hodari kwa nguvu.” Kwa hiyo, wahamishwa Wayahudi wana sababu ya kuwa na tumaini. Muumba, anayeziongoza nyota, ana nguvu za kuwategemeza watumishi wake.

      25. Twaweza kuitikiaje mwaliko wa Mungu ulioandikwa kwenye Isaya 40:26, na kukiwa na matokeo gani?

      25 Ni nani kati yetu awezaye kuukataa mwaliko wa Mungu ulioandikwa kwenye Isaya 40:26: “Inueni macho yenu juu, mkaone”? Uvumbuzi mbalimbali wa waastronomia wa leo umeonyesha kuwa mbingu zilizojaa nyota ni za ajabu hata zaidi kuliko zilivyoonekana katika siku ya Isaya. Waastronomia wanaotazama mbinguni wakitumia darubini kali wanakadiria kuwa ulimwengu unaoonekana una makundi ya nyota yapatayo bilioni 125. Lahaula, kwa makadirio fulani, mojawapo la makundi hayo liitwalo Kilimia, lina nyota zaidi ya bilioni 100! Kujua hayo kwapaswa kutuchochea tumstahi Muumba wetu kutoka moyoni na kulitumaini kabisa neno lake la ahadi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki