-
Wenye Kufariji UnaokuhusuUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Je, miungu ya mataifa inaweza kutoa unabii kwa usahihi na hivyo ithibitishe kwamba ina ujuzi unaopita ule wa kawaida? Ikiwa inaweza, basi kwapaswa kuwe na matokeo fulani, mema ama mabaya, ya kuunga mkono madai yao. Ingawa hivyo, ukweli ni kwamba miungu-sanamu haina uwezo wa kutimiza lolote, nayo ni kama kazi bure.
23. Ni kwa nini Yehova, kupitia manabii wake, aliendelea sana kulaumu sanamu vikali?
23 Siku zetu, huenda wengine wakajiuliza ni kwa nini Yehova, kupitia Isaya na manabii wenzake, alitumia muda wote huo kulaumu vikali upumbavu wa kuabudu sanamu. Huenda wengi leo wakaonekana wanatambua wazi kwamba sanamu zilizotengenezwa na wanadamu ni bure. Hata hivyo, mfumo wa imani za uwongo ukiisha kuanzishwa na kukubaliwa mahali pengi, ni vigumu kuung’oa akilini mwa wale wanaouamini. Imani nyingi za wakati wetu ni upumbavu kama tu upumbavu wa kuamini kwamba mifano isiyo na uhai ni miungu kikweli. Na bado watu hushikilia imani hizo hata kama kuna hoja za kusadikisha kwamba imani hizo si kweli. Ni baada tu ya kusikia ukweli tena na tena kwamba wengine huguswa moyo kuiona hekima ya kumtumaini Yehova.
-
-
Wenye Kufariji UnaokuhusuUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Tujulisheni yatakayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu; naam, tendeni mema au tendeni mabaya, ili tujipime, tukaone pamoja.
-