-
“Mteule Wangu, Ambaye Nafsi Yangu Imependezwa Naye”!Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
19, 20. (a) Ni lazima wimbo gani uimbwe? (b) Ni nani leo wanaomwimbia Yehova wimbo wa sifa?
19 Isaya anaandika hivi: “Mwimbieni BWANA wimbo mpya, na sifa zake tokea mwisho wa dunia; ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, na visiwa, nao wakaao humo.
-
-
“Mteule Wangu, Ambaye Nafsi Yangu Imependezwa Naye”!Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
20 Wakaaji wa miji, wa vijiji jangwani, wa visiwa, hata wa “Kedari,” au kambi zilizopigwa katika majangwa—watu kila mahali—wanahimizwa wamwimbie Yehova wimbo wa sifa. Inasisimua kama nini kwamba katika siku zetu mamilioni ya watu wameitikia mwito huo wa unabii! Wameikubali kweli ya Neno la Mungu kwa moyo, wakamkubali Yehova awe Mungu wao. Watu wa Yehova wanaimba wimbo huo mpya—wakisema Yehova anastahili utukufu—katika nchi zaidi ya 230. Inasisimua kama nini kuimba katika kwaya hiyo ya tamaduni, lugha, na rangi nyingi sana!
-