-
Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Je! ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu?
-
-
Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
9. Yehova amelitunzaje taifa lake kama shamba la mizabibu lenye kuthaminiwa?
9 Yehova ‘alilipanda’ taifa lake katika nchi ya Kanaani na kuwapa sheria na kanuni zake, zilizokuwa kama ukuta wa kuwalinda ili mataifa mengine yasiwafisidi. (Kutoka 19:5, 6; Zaburi 147:19, 20; Waefeso 2:14) Pamoja na hayo, Yehova aliwapa waamuzi, makuhani, na manabii wa kuwafundisha. (2 Wafalme 17:13; Malaki 2:7; Matendo 13:20) Israeli ilipotishwa kwa uvamizi wa kijeshi, Yehova aliinua wakombozi. (Waebrania 11:32, 33) Kwa kufaa, Yehova auliza: “Je! ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda?”
-