-
Mungu wa Kweli Anatabiri UkomboziUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
10, 11. Kwa nini Yehova anaiona mifano kuwa aibu?
10 Sasa Isaya anaeleza ubatili wa mifano isiyo hai na aibu inayowangoja wale wanaoifanyiza: “Wachongao sanamu [“mifano,” “NW”], wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.
-
-
Mungu wa Kweli Anatabiri UkomboziUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
11 Kwa nini Mungu anaiona mifano hiyo kuwa ya aibu sana? Kwanza, haiwezekani kumwakilisha Mweza Yote kwa kutumia vitu halisi vinavyoonekana. (Matendo 17:29) Tena, kuabudu kiumbe badala ya Muumba ni kukaidi Uungu wa Yehova. Na je, kufanya hivyo si kushusha heshima ya mwanadamu, aliyeumbwa “kwa mfano wa Mungu”?—Mwanzo 1:27; Waroma 1:23, 25.
-