-
Mungu wa Kweli Anatabiri UkomboziUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
12, 13. Kwa nini mwanadamu hawezi kuunda mfano wowote unaostahili kuabudiwa?
12 Je, kitu halisi kinaweza kupata utakatifu kwa njia fulani eti kwa sababu kimeundwa ili kiabudiwe? Isaya anatukumbusha kwamba kutengeneza mfano ni kazi ya binadamu tu. Vyombo na maarifa yanayotumiwa na mtengeneza-mifano ni sawa na vile vya fundi mwingine yeyote: “Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kazi kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia.
-
-
Mungu wa Kweli Anatabiri UkomboziUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
13 Mungu wa kweli aliumba vitu vyote vilivyo hai juu ya dunia hii, kutia na mwanadamu. Viumbe vyenye fahamu vinashuhudia vizuri sana Uungu wa Yehova, lakini ni wazi kuwa viumbe vyote vya Yehova vina cheo kidogo kuliko yeye. Je, inawezekana mwanadamu afanye makubwa zaidi ya hayo? Je, anaweza kutengeneza kitu kilicho na cheo kikubwa kuliko yeye mwenyewe—kiwe na cheo kikubwa sana hata kistahili ujitoaji wake? Mwanadamu anapotengeneza mfano, yeye huchoka, huona njaa, na kiu. Hayo ni mapungufu ya kibinadamu, lakini angalau yanaonyesha kwamba mwanadamu huyo yuko hai.
-