-
Mungu wa Kweli Anatabiri UkomboziUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Upeo wa Kutahini Uungu
19, 20. (a) Yehova anafikisha kesi yake kwenye upeo kwa njia gani? (b) Yehova anawatolea watu wake unabii wa mambo gani yenye kuchangamsha, na ni nani atakuwa mwakilishi wake wa kuyatimiza?
19 Yehova sasa analeta hoja yake ya kisheria kwenye upeo mpevu. Yeye mwenyewe anakaribia kuujibu mtihani mkali kupita wote wa Uungu wake, yaani, kama kweli anaweza kutabiri wakati ujao kwa usahihi. Msomi mmoja wa Biblia aliiita mistari mitano inayofuata ya Isaya sura ya 44, “shairi lisilo na kifani la Mungu wa Israeli,” yule Muumba mmoja, tena mmoja tu, aliye Mfunuaji pekee wa wakati ujao na tumaini la ukombozi wa Israeli.
-
-
Mungu wa Kweli Anatabiri UkomboziUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
20 “BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?
-