-
Yehova—“Mungu Mwenye Haki, Mwokozi”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma;
-
-
Yehova—“Mungu Mwenye Haki, Mwokozi”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Kisha, Koreshi ashambuliapo Babiloni, Yehova atahakikisha kwamba milango ya jiji imeachwa wazi, aifanye iwe ovyo kama malango ambayo yamekwisha kuvunjwa-vunjwa. Ataenda mbele ya Koreshi, akitandaza vipingamizi vyote.
-
-
Yehova—“Mungu Mwenye Haki, Mwokozi”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
5, 6. Unabii wa anguko la Babiloni unatimia wakati gani na jinsi gani?
5 Mwaka wa 539 K.W.K.—kama miaka 200 baada ya Isaya kuandika unabii huu—kwa kweli Koreshi anawasili kwenye kuta za Babiloni kushambulia jiji hilo. (Yeremia 51:11, 12) Hata hivyo, Wababiloni hawajali. Wanaona kwamba jiji lao halishindiki. Kuta zake ndefu zimeinuka sana juu ya mahandaki ya kina kirefu yaliyojaa maji ya Mto Eufrati, ambao ni sehemu ya mfumo wa kinga za jiji. Miaka zaidi ya mia moja ndiyo hiyo, na hakuna adui amefaulu kuipiga Babiloni dafrao! Kwa kweli, Belshaza, aliye mtawala mkazi wa Babiloni, anajiona salama salimini, hata anakula karamu na washiriki wa baraza lake. (Danieli 5:1) Usiku huo—huo usiku wa Oktoba 5/6—Koreshi akamilisha mbinu murua ya ushambulizi wa kijeshi.
6 Kwenye maji ya upande wa juu kutoka Babiloni, wahandisi wa Koreshi wamepasua njia kuupita ukingo wa Mto Eufrati, wakabadili mkondo wa maji yake mengi, na sasa hayatiririki tena kusini kuelekea jijini. Muda si muda, maji ya mto yaliyo ndani ya Babiloni na vizingo vyake yamepunguka sana hivi kwamba vikosi vya Koreshi vyaweza kupita chubwichubwi katika sakafu ya mto, kuelekea kitovu cha jiji hilo. (Isaya 44:27; Yeremia 50:38) Jamani, malango kando ya mto yako wazi, sawasawa na utabiri wa Isaya. Majeshi ya Koreshi yamiminika Babiloni kama siafu, yanaiteka kasri, yanamwua Mfalme Belshaza. (Danieli 5:30) Kwa usiku mmoja, ushindi wakamilika. Babiloni kaanguka, unabii katimizwa neno kwa neno.
-