Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 17. Ni mwenendo gani mwovu unaoshutumiwa katika ole wa kwanza wa Isaya?

      17 Katika mstari wa 8, Isaya haendelei kunukuu maneno ya Yehova. Huku akishutumu baadhi ya “zabibu-mwitu” zinazozaliwa katika Yuda, yeye binafsi atangaza ole wa kwanza kati ya ole sita: “Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hata hapana nafasi tena, nanyi hamna budi kukaa peke yenu kati ya nchi!

  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 5:8

  • Ole kwa Shamba la Mizabibu Lisilo na Uaminifu!
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 18, 19. Watu wa siku ya Isaya wanapuuzaje sheria za Yehova kuhusu mali, na matokeo yatakuwa nini kwao?

      18 Katika Israeli ya kale, nchi yote ilikuwa mali ya Yehova. Kila familia ilipata urithi kutoka kwa Mungu, ambao wangeweza kuukodisha au kuukopesha, ila hawangeweza kuuuza “kabisa kabisa.” (Mambo ya Walawi 25:23) Sheria hiyo ilizuia utumiaji mbaya, kama vile kuhodhi mashamba. Hiyo pia ilizilinda familia zisiwe maskini hohehahe. Ijapokuwa hivyo, watu fulani katika Yuda walikuwa wakivunja kwa pupa sheria za Mungu juu ya mali. Mika aliandika hivi: “Nao hutamani mashamba, na kuyashika; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na nyumba yake, naam, mtu na urithi wake.” (Mika 2:2) Lakini Mithali 20:21 yaonya hivi: “Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki