-
Yehova—“Mungu Mwenye Haki, Mwokozi”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
-
-
Yehova—“Mungu Mwenye Haki, Mwokozi”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Maneno ya Mungu yenyewe yanategemeka, lakini yanategemeka hata zaidi Yehova anapoyaongezea kiapo chake kuyathibitisha. (Waebrania 6:13) Kwa haki, yeye hutaka wale wanaotamani upendeleo wake wamwonyeshe unyenyekeo (“kila goti litapigwa”) na kuwajibika mbele zake (“kila ulimi utaapa”).
-
-
Yehova—“Mungu Mwenye Haki, Mwokozi”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Katika barua yake kwa Waroma, mtume Paulo alinukuu tafsiri ya Septuagint ya Isaya 45:23 kuonyesha kwamba hatimaye kila mtu aliye hai atakiri enzi kuu ya Mungu na kusifu jina lake kwa uendelevu.—Waroma 14:11; Wafilipi 2:9-11; Ufunuo 21:22-27.
-