-
Yehova Hutufundisha kwa Faida YetuUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
15. Yehova “amempenda” Koreshi jinsi gani na kwa kusudi gani?
15 Mwaliko mzito unaelekezwa kwa Wayahudi na hata kwa watu wasio Wayahudi: “Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.
-
-
Yehova Hutufundisha kwa Faida YetuUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Yehova peke yake ndiye mwenye nguvu zote na anaweza kutabiri matukio kwa usahihi. Hakuna sanamu yoyote miongoni “mwao,” yaani miongoni mwa sanamu hizo ovyo, inayoweza kueleza mambo hayo. Ni Yehova, wala si sanamu hizo, ambaye “amempenda” Koreshi—yaani, Yehova amemchagua kwa kusudi fulani hususa. (Isaya 41:2; 44:28; 45:1, 13; 46:11) Yeye ametangulia kumwona Koreshi akitokea katika mandhari ya ulimwengu, akamtaja wazi kuwa ndiye mshindi atakayeteka Babiloni wakati ujao.
-