-
Biblia Kitabu cha Unabii Sahihi Sehemu ya 4Amkeni!—2012 | Agosti
-
-
Ilitabiriwa Kristo Angeteseka
Unabii wa 1: “Mgongo wangu niliwapa washambuliaji.”—Isaya 50:6.c
Utimizo: Katika mwaka wa 33 W.K., Wayahudi, waliokuwa maadui wa Yesu, walimleta mbele ya Gavana Mroma Pontio Pilato ili ahukumiwe. Akitambua kwamba Yesu hakuwa na hatia, gavana huyo alijaribu kumwachilia. Hata hivyo, kwa kuwa Wayahudi walisisitiza kwamba Yesu auawe, Pilato “akatoa hukumu ili dai lao litimizwe” na akamtoa Yesu ili atundikwe mtini. (Luka 23:13-24) Hata hivyo, kwanza “Pilato akamchukua Yesu na kumpiga mijeledi,” au aliagiza apigwe viboko. (Yohana 19:1) Kama Isaya alivyotabiri, Yesu hakujizuia lakini ‘aliwapa washambuliaji wake mgongo wake.’
Historia inafunua nini?
● Historia inathibitisha kwamba kwa kawaida Waroma waliwapiga wafungwa wao mijeledi kabla ya kuwaua. Kulingana na kitabu kimoja cha marejezo, “watu walipigwa kwa kutumia mjeledi uliokuwa na kamba kadhaa za ngozi zilizokuwa na vipande vya madini ya risasi au vyuma vyenye ncha kali. Mfungwa . . . alipigwa kwenye mgongo ulio wazi . . . hadi ngozi yake iliporaruka. Nyakati nyingine alikufa.” Hata hivyo, Yesu hakufa kutokana na kipigo hicho.
-
-
Biblia Kitabu cha Unabii Sahihi Sehemu ya 4Amkeni!—2012 | Agosti
-
-
c Muktadha unaonyesha kwamba neno “niliwapa” katika unabii huu linarejelea Kristo. Kwa mfano, mstari wa 8 unasema: “Yeye [Mungu] anayenitangaza mimi [Yesu Kristo] kuwa mwadilifu yupo karibu.” Alipokuwa duniani, Yesu tu ndiye aliyekuwa mwadilifu, au bila dhambi, machoni pa Mungu.—Waroma 3:23; 1 Petro 2:21, 22.
-