Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Faraja kwa Watu wa Mungu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 7, 8. (a) Yehova ana maana gani anapotoa mwito watu watege sikio kumsikiliza? (b) Kwa nini ni muhimu Yuda wamsikize Yehova?

      7 Yehova anaomba tena watu wake wamsikilize, akisema hivi: “Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, nami nitaistarehesha hukumu yangu iwe nuru ya mataifa.

  • Faraja kwa Watu wa Mungu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 51:4,

  • Faraja kwa Watu wa Mungu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 8 Yehova anapotoa mwito watu watege sikio kumsikiliza, kinachohitajiwa si kuusikia ujumbe wake tu. Inamaanisha kutega sikio kwa lengo la kuyatenda yale yanayosikiwa. (Zaburi 49:1; 78:1) Ni lazima taifa lifahamu kwamba Yehova ndiye Chanzo cha maagizo, haki, na wokovu. Yeye peke yake ndiye Chanzo cha nuru ya kiroho. (2 Wakorintho 4:6) Yeye ndiye Hakimu anayekata kauli ya mwisho kuhusu wanadamu. Sheria na maamuzi ya hukumu zitokazo kwa Yehova ni nuru kwa wale wanaojiruhusu waongozwe nazo.—Zaburi 43:3; 119:105; Mithali 6:23.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki