-
Faraja kwa Watu wa MunguUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu.” (Isaya 51:15, 16)
-
-
Faraja kwa Watu wa MunguUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
20. Yehova anaporudisha Sayuni katika hali ya kwanza, ni “mbingu” zipi na “dunia” ipi zitakazotokea, naye atatamka maneno gani yenye kufariji?
20 Bado Wayahudi ni watu wa agano la Mungu, na Yehova anawahakikishia kwamba watairudia nchi yao, ili wakaishi tena chini ya Sheria. Wakiwa huko, watajenga upya Yerusalemu na hekalu lake, warudie madaraka yao wakiwa chini ya agano aliloagana nao kupitia Musa. Nchi ianzapo kukaliwa upya na Waisraeli waliorudishwa pamoja na mifugo yao, “dunia mpya” itatokea. “Mbingu mpya,” ambazo ni mfumo mpya wa kiserikali, zitawekwa juu ya hiyo “dunia mpya.” (Isaya 65:17-19, NW; Hagai 1:1, 14) Yehova ataiambia tena Sayuni: “Ninyi ni watu wangu.”
-