Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Imbeni Pamoja kwa Shangwe’!
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi.” (Isaya 52:5, 6)

  • ‘Imbeni Pamoja kwa Shangwe’!
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 9, 10. Watu wa agano la Mungu wa nyakati za kisasa wamepata uelewevu gani wa kina kirefu zaidi kuhusu viwango vya Yehova na jina lake?

      9 Koreshi Mkubwa Zaidi, Yesu Kristo, alipowaweka huru watu wa agano la Mungu kutoka utekwa wa Babiloni Mkubwa mwaka wa 1919, waliyaelewa matakwa ya Yehova vizuri zaidi. Tayari walikuwa wamejisafisha kwa kuondoa mafundisho mengi ya Jumuiya ya Wakristo yaliyo na mizizi katika upagani wa nyakati zilizoutangulia Ukristo, kama vile Utatu, kutokufa kwa nafsi, na mateso ya milele katika helo yenye moto. Sasa walianza kujiondolea kabisa dalili zote za mavutano ya Kibabiloni. Pia wakaja kuutambua umuhimu wa kudumisha msimamo wa kutokuwamo kabisa katika mambo ya uzalendo wa ulimwengu huu. Hata walitaka kujitakasa kwa kuondoa hatia yoyote ya damu ambayo huenda ikawa baadhi yao walijiletea.

      10 Pia watumishi wa kisasa wa Mungu walipata uelewevu wa kina kirefu zaidi juu ya umuhimu wa jina la Yehova. Mwaka wa 1931 walikubali kulitwaa jina Mashahidi wa Yehova, na hivyo wakatangaza peupe kwamba wanaunga mkono Yehova na jina lake. Zaidi ya hilo, kwa kuchapisha Biblia ya New World Translation tangu mwaka wa 1950, Mashahidi wa Yehova wamelirudisha jina la Mungu mahali pake katika Biblia. Naam, wao wamekuja kuthamini jina la Yehova na wanalijulisha mpaka miisho ya dunia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki