-
Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa KimesiyaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.” (Isaya 52:14a, 15) Kwa maneno hayo, Isaya anaeleza, si juu ya kutokea kwa Mesiya mara ya kwanza, bali juu ya kukabiliana kwake na watawala wa kidunia mara ya mwisho.
-
-
Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa KimesiyaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Ni kweli kuwa watawala wa kibinadamu hawatamwona kihalisi Yesu aliyetukuzwa. Lakini wataona dalili za waziwazi za kuthibitisha nguvu zake akiwa Mpiganaji wa kimbingu mwenye kumtetea Yehova. (Mathayo 24:30) Watalazimika kulifahamu jambo ambalo hawajawahi kusikia likisimuliwa na viongozi wa kidini—kwamba Yesu ndiye Mfikilizaji wa hukumu za Mungu! Mtumishi aliyekwezwa watakayekutana naye atatenda kwa njia ambayo hawaitazamii.
-