Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa Kimesiya
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Kuteseka kwa Mesiya kulifikia upeo alipodungwa, akachubuliwa, na kujeruhiwa. Maneno hayo yanakazia sana kifo chenye jeuri na maumivu. Lakini kifo chake kina nguvu za kufunika dhambi; kinaandaa msingi wa kuwarudishia hali njema wale wanaotanga-tanga katika makosa na dhambi, kuwasaidia waweze kupata amani pamoja na Mungu.

  • Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa Kimesiya
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Hata hivyo, kumbuka kwamba hakuteseka kwa sababu ya dhambi zozote alizozitenda mwenyewe. “Kristo aliteseka kwa ajili yenu,” anasema Petro, “akiwaachia kigezo ili nyinyi mfuate hatua zake kwa ukaribu. Yeye hakufanya dhambi, wala udanganyo haukupatikana kinywani mwake. Yeye mwenyewe alichukua dhambi zetu katika mwili wake mwenyewe juu ya mti, ili tupate kuachana kabisa na dhambi na kuishi kuelekea uadilifu. Na ‘kwa mapigo yake mliponywa.’” (1 Petro 2:21, 22, 24)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki