-
Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa KimesiyaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
“Bwana Aliridhika Kumchubua”
30. Yehova aliridhika kumchubua Yesu katika maana gani?
30 Kisha Isaya anasema jambo la kugutusha: “BWANA aliridhika kumchubua; amemhuzunisha; utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi [“toleo la hatia,” “NW”], ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
-
-
Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa KimesiyaUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Kwa kweli ingewezekanaje Yehova aridhike kumwona mtumishi huyu mwaminifu akiwa amechubuka? Ni wazi kwamba si Yehova binafsi aliyemtesa Mwana wake mpendwa. Adui za Yesu walikuwa na lawama kamili kwa yale waliyomtenda. Lakini Yehova aliwaruhusu watende ukatili. (Yohana 19:11) Kwa sababu gani? Hakika huyo Mungu wa hisia-mwenzi na huruma nyororo aliumia kumwona Mwanawe asiye na hatia akiteseka. (Isaya 63:9; Luka 1:77, 78) Hakika Yehova hakuchukizwa na Yesu kwa vyovyote. Hata hivyo, Yehova aliridhishwa na hiari ya Mwanawe kuteseka kwa ajili ya baraka zote ambazo zingetokana na mateso yake.
31. (a) Yehova aliitoaje nafsi ya Yesu iwe “toleo la hatia”? (b) Baada ya taabu zote zilizompata Yesu akiwa mwanadamu, ni hakika kwamba yeye anaridhishwa na jambo gani hasa?
31 Kwanza, Yehova aliitoa nafsi ya Yesu iwe “toleo la hatia.” Hivyo basi, Yesu alipopaa kurudi mbinguni, aliingia mbele za Yehova, akiwa na ubora wa uhai wake wa kibinadamu uliotolewa dhabihu uwe toleo la hatia, na Yehova alifurahi kuukubali kwa niaba ya wanadamu wote. (Waebrania 9:24; 10:5-14) Yesu alijipatia “uzao” kupitia toleo lake la hatia. Akiwa “Baba wa milele,” anaweza kuwapa uhai—uhai wa milele—wale wanaodhihirisha imani katika damu yake iliyomwagwa. (Isaya 9:6)
-