Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa Kimesiya
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki [“ataletea wengi msimamo wenye uadilifu,” “NW”]; naye atayachukua maovu yao.” (Isaya 53:10, 11)

  • Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa Kimesiya
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Baada ya taabu zote zilizompata Yesu akiwa nafsi ya kibinadamu, yeye anaridhika kama nini kuwa na tazamio la kuwakomboa wanadamu kutoka katika dhambi na kifo! Na bila shaka anaridhika hata zaidi kujua kwamba uaminifu wake wa maadili ulimwandalia Baba yake wa kimbingu jibu kwa ajili ya dhihaka kali za Adui Yake, Shetani Ibilisi.—Mithali 27:11.

      32. Yesu anatumia “maarifa” gani ‘kuletea wengi msimamo wenye uadilifu,’ na ni nani wanaopata msimamo huo?

      32 Baraka nyingine inayotokana na kifo cha Yesu ni kwamba analetea “wengi msimamo wenye uadilifu,” hata sasa. Isaya anasema kwamba anafanya hivyo “kwa maarifa yake.” Ushuhuda unaonyesha kwamba hayo ni maarifa ambayo Yesu alijipatia kwa kuwa mwanadamu na kuteseka isivyo haki kwa kumtii Mungu. (Waebrania 4:15) Baada ya kuteseka hadi kifo, Yesu aliweza kuandaa dhabihu iliyohitajiwa ili kuwasaidia wengine wapate msimamo wenye uadilifu. Ni nani wanaopata msimamo huo wenye uadilifu? Kwanza, ni wafuasi wake watiwa-mafuta. Kwa sababu wanadhihirisha imani katika dhabihu ya Yesu, Yehova anawatangaza kuwa waadilifu kwa tazamio la kuwafanya wawe wanawe, na kuwafanya warithi-washirika na Yesu. (Waroma 5:19; 8:16, 17) Halafu “umati mkubwa” wa “kondoo wengine” unadhihirisha imani katika damu ya Yesu iliyomwagwa na kufurahia msimamo wenye uadilifu wakiwa na tazamio la kuwa rafiki za Mungu na kuwa waokokaji wa Har-Magedoni.—Ufunuo 7:9; 16:14, 16; Yohana 10:16; Yakobo 2:23, 25.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki