Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu Ni Yehova”
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 1
    • Isaya 6:1-3

  • “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu Ni Yehova”
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 1
    • Isaya anajawa na woga na heshima si kwa sababu ya mambo anayoona tu, bali pia kwa sababu ya mambo anayosikia. Maserafi wanaunganisha sauti zao na kuimba pamoja. Isaya anaandika: “Huyu akamwita yule na kusema: ‘Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Yehova wa majeshi.’” (Mstari wa 3) Neno la Kiebrania linalotafsiriwa “mtakatifu” linamaanisha usafi na utakato. Neno hilo pia lina maana ya “kuwa huru na kutengwa kabisa na dhambi.” Katika wimbo huo ambao inaelekea kikundi kimoja cha maserafi kinaimba huku kingine kikiitikia, maserafi hao wanataja neno “mtakatifu” mara tatu, wakikazia kwamba Yehova ni mtakatifu kwa njia isiyo na kifani. (Ufunuo 4:8) Kwa hiyo, utakatifu ni sifa ya kipekee ya utu wa Mungu. Kwa kweli, Yehova ni safi kabisa na hana doa lolote la uovu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki