-
Unafiki Wafichuliwa!Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Kufunga Kula kwa Njia ya Unafiki
5. Wayahudi wanajaribu kukubaliwa na Mungu kwa kufanya nini, na Yehova anaitikiaje?
5 Wayahudi wanajitahidi kukubaliwa na Mungu kwa kufuata desturi ya kufunga kula, lakini uchaji wao wa kusingizia unazidi tu kuwatenganisha na Yehova. Na inaonekana wanatatanika fikira, kwani wanauliza hivi: “Ya nini tufunge chakula usipoona? Ya nini tujitese usipoangalia?” Naye Yehova anawaambia hivi bila kuwaficha neno: “Siku za kufunga mwafanya biashara [“mlikuwa mkijifurahisha,” “NW”], na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
-
-
Unafiki Wafichuliwa!Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
6. Ni vitendo gani vya Wayahudi vinavyoonyesha kwamba wanafunga kwa unafiki?
6 Watu hao wanafunga kula, wanajifanya wenye haki, na hata wanaomba Yehova awafanyie hukumu za haki, huku wao wakifuatia raha kwa ubinafsi na kuendesha biashara zao.
-