Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mungu Yumo Katika Hekalu Lake Takatifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 22 Kama vile Isaya, Yesu alitimiza kwa uaminifu kazi aliyopewa naye akakabili itikio lilelile. Wayahudi katika siku ya Yesu hawakuwa na nia ya kuukubali ujumbe huo kama wale aliohubiria nabii Isaya. (Isaya 1:4) Yesu alitumia vielezi katika huduma yake. Hilo liliwachochea wanafunzi wake kuuliza hivi: “Ni kwa nini wewe huwaambia kwa utumizi wa vielezi?” Yesu akajibu: “Nyinyi mmeruhusiwa kuzielewa siri takatifu za ufalme wa mbingu, lakini watu hao hawakuruhusiwa. Hii ndiyo sababu nawaambia kwa utumizi wa vielezi, kwa sababu, wakitazama, watazama bure, na wakisikia, wasikia bure, wala hawapati maana yake; na kuwaelekea wao unabii wa Isaya unapata utimizo, ambao husema, ‘Kusikia, mtasikia lakini kwa vyovyote hamtapata maana yake; na, kutazama, mtatazama lakini kwa vyovyote hamtaona. Kwa maana moyo wa watu hawa umekuwa usioitikia, na kwa masikio yao wamesikia bila itikio, nao wamefunga macho yao; ili wasipate kuona kamwe kwa macho yao na kusikia kwa masikio yao na kupata maana kwa mioyo yao na kurudi, nami niwaponye.’”—Mathayo 13:10, 11, 13-15; Marko 4:10-12; Luka 8:9, 10.

      23 Kwa kunukuu kitabu cha Isaya, Yesu alikuwa akionyesha kuwa unabii huo una utimizo fulani katika siku yake. Mtazamo wa moyo wa watu kwa jumla ulikuwa kama wa Wayahudi katika siku ya Isaya. Walijifanya vipofu na viziwi wasipate ujumbe wake nao vivyo hivyo wakaharibiwa. (Mathayo 23:35-38; 24:1, 2)

  • Mungu Yumo Katika Hekalu Lake Takatifu
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 24. Paulo alionyesha utimizo gani wa unabii wa Isaya, na jambo hilo laonyesha nini?

      24 Karibu mwaka wa 60 W.K., mtume Paulo alikuwa katika kizuizi cha nyumbani huko Roma. Huko, yeye alipanga mkutano na “watu walio wakubwa wa Wayahudi” pamoja na wengine, naye akawapa “ushahidi kamili kuhusiana na ufalme wa Mungu.” Wengi wao walipokataa kukubali ujumbe wake, Paulo alieleza kuwa huo ni utimizo wa unabii wa Isaya. (Matendo 28:17-27; Isaya 6:9, 10) Kwa hiyo wanafunzi wa Yesu walitimiza utume unaofanana na ule wa Isaya.

      25. Mashahidi wa Mungu leo wametambua nini, nao huitikiaje?

      25 Vivyo hivyo, Mashahidi wa Yehova leo hutambua kwamba Yehova Mungu yumo katika hekalu lake takatifu. (Malaki 3:1) Kama vile Isaya, wao husema: “Mimi hapa, nitume mimi.” Wao hutangaza kwa bidii ujumbe unaotoa onyo juu ya mwisho unaokaribia wa mfumo huu wa mambo ulio mwovu. Hata hivyo, kama Yesu alivyoonyesha, ni watu wachache tu wanaofungua macho na masikio yao ili kuona na kusikia na kupata kuokolewa. (Mathayo 7:13, 14) Bila shaka, wenye furaha ni wale wanaoelekeza mioyo yao ipate kusikiliza na “kuponywa”!—Isaya 6:8, 10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki