-
Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.
-
-
Ni Nani Awezaye Kusimama Dhidi ya mkuu wa Wakuu?Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
14. Malaika Gabrieli alisema nini juu ya utendaji mbalimbali wa ile pembe ndogo ya mfano, nayo ingepatwa na nini?
14 Kabla hatujaweza kuelewa maana ya maneno yaliyotoka kunukuliwa, lazima tumsikilize malaika wa Mungu. Baada ya kutaja juu ya kupata mamlaka kwa zile falme nne zilizotokana na milki ya Aleksanda, malaika Gabrieli asema hivi: “Wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama. Na nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe; naye ataharibu kiasi cha kustaajabisha watu, na kufanikiwa, na kutenda apendavyo; naye atawaangamiza hao walio hodari na watu watakatifu.
-