Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa Mungu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • “Majuma matatu kamili,” au siku 21 za kuomboleza na kufunga ni kipindi kirefu isivyo kawaida. Yaonekana aliacha kuomboleza “siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza.” (Danieli 10:4) Kwa hiyo, kipindi cha kufunga kwa Danieli kilitia ndani Sikukuu ya Kupitwa, iliyoadhimishwa siku ya 14 ya mwezi wa kwanza, Nisani, na ule msherehekeo wa siku saba uliofuata wa mkate usiotiwa chachu.

  • Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa Mungu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 9, 10. (a) Danieli alikuwa wapi alipoona ono? (b) Fafanua kile ambacho Danieli aliona kwenye ono.

      9 Danieli hatamaushwi. Anatuambia kifuatacho kutokea, akisema hivi: “Nilipokuwa kando ya ule mto mkubwa, Hidekeli; naliinua macho yangu, nikatazama, na kumbe, mtu aliyevikwa nguo za kitani, viuno vyake vimefungwa dhahabu safi ya Ufazi.” (Danieli 10:4, 5) Hidekeli ulikuwa mmojawapo wa mito minne iliyotoka kwenye bustani ya Edeni. (Mwanzo 2:10-14) Katika Kiajemi cha Kale, Hidekeli uliitwa Tigra, litokapo jina la Kigiriki, Tigris. Eneo lililo kati ya Hidekeli na Eufrati lilikuja kuitwa Mesopotamia, yaani “Nchi Iliyo Katikati ya Mito.” Hilo lathibitisha kwamba Danieli alipoona ono hilo, bado alikuwa Babilonia, ingawa huenda hakuwa katika jiji la Babiloni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki