Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa Mungu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 10 Danieli aliona ono lililoje! Ni wazi kwamba hakuona mtu wa kawaida alipoinua macho yake. Danieli alimfafanua vilivyo: “Mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.”—Danieli 10:6.

  • Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa Mungu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 13 Danieli alitiwa kicho pia na sura ya mjumbe huyo—kung’aa kwake kana kwamba alikuwa na mwili wa vito, kumulika sana kwa uso wake mwangavu, uwezo wenye kupenya wa macho yake yaliyo kama taa za moto, na mng’ao wa mikono na miguu yake yenye nguvu. Hata sauti yake yenye kuamuru ilikuwa yenye kutia kicho. Yote hayo yaonyesha waziwazi kwamba alikuwa na uwezo upitao wa kibinadamu. ‘Mtu huyo aliyevikwa nguo za kitani’ hakuwa mwingine ila malaika mwenye wadhifa mkubwa, aliyetumikia katika kuwapo kutakatifu kwa Yehova, alipotoka na ujumbe.a

  • Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa Mungu
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • a Ingawa malaika huyo hatajwi kwa jina, yaonekana ndiye yuleyule ambaye sauti yake ilisikiwa ikimwagiza Gabrieli amsaidie Danieli kuhusu lile ono ambalo alikuwa ametoka tu kuona. (Linganisha Danieli 8:2, 15, 16 na Danieli 12:7, 8.) Isitoshe, Danieli 10:13 huonyesha kwamba Mikaeli, “mmoja wa hao wakuu wa mbele,” alikuja kumsaidia malaika huyo. Kwa hiyo, malaika huyo asiyetajwa kwa jina lazima alikuwa na pendeleo la kufanya kazi bega kwa bega na Gabrieli na Mikaeli.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki