Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wale Wafalme Wawili Wabadilika
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 7, 8. (a) Ni nani aliyechukua mahali pa Augusto akiwa mfalme wa kaskazini? (b) Kwa nini Kaisari Augusto alimpa mwandamizi wake “heshima ya ufalme” kwa shingo upande?

      7 Akiendelea na unabii huo, malaika asema hivi: “Badala yake [Augusto] atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza [“kunyakua ufalme kwa hila,” BHN].

  • Wale Wafalme Wawili Wabadilika
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 8 “Mtu astahiliye kudharauliwa” alikuwa Kaisari Tiberio, mwana wa Livia, mke wa tatu wa Augusto. (Ona “Mmoja Aheshimiwa, Yule Mwingine Adharauliwa,” kwenye ukurasa wa 248.) Augusto alimchukia mwana wake wa kambo kwa sababu ya tabia yake mbaya wala hakutaka awe Kaisari baada yake. Alimpa “heshima ya ufalme” shingo upande baada ya watu wote ambao wangeweza kuwa Kaisari kufa. Augusto alimwasilisha Tiberio mwaka wa 4 W.K. na kumfanya awe mrithi wa ufalme. Baada ya Augusto kufa, Tiberio mwenye umri wa miaka 54—mwenye kudharauliwa—‘akasimama,’ akitwaa mamlaka ya kuwa maliki wa Roma na mfalme wa kaskazini.

      9. Tiberio ‘alinyakuaje ufalme kwa hila’?

      9 “Tiberio,” yasema The New Encyclopædia Britannica, “alitumia hila dhidi ya Seneti wala hakuiruhusu imteue awe maliki kwa zaidi ya mwezi mmoja [baada ya Augusto kufa].” Aliiambia Seneti kwamba hakuna mtu yeyote ila Augusto aliyekuwa na uwezo wa kubeba mzigo wa kutawala Milki ya Roma na akawaomba maseneta waweke kikundi cha watu kimiliki badala ya mtu mmoja. “Bila kunuia kukubali aliyosema,” akaandika mwanahistoria Will Durant, “Seneti ilibembelezana-bembelezana naye mpaka hatimaye akaikubali mamlaka hiyo.” Durant alisema hivi pia: “Pande zote mbili zilikuwa zikijifanya. Tiberio alitaka kuwa maliki wa Roma, la sivyo angalipata njia ya kuuhepa umaliki; Seneti ilimhofu na kumchukia, lakini haikutaka tena kuwa jamhuri, kama ile ya kale, ambayo ilitegemea mabunge ya watawala ya kuwaziwa tu.” Kwa hiyo, Tiberio ‘akaunyakua ufalme kwa hila.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki