-
Wale Wafalme Wawili WabadilikaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Naam, walao sehemu ya chakula chake watamwangamiza, na jeshi lake litagharikishwa; na wengi wataanguka wameuawa.”—Danieli 11:25, 26.
-
-
Wale Wafalme Wawili WabadilikaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Mwaka wa 275 W.K., alifunga safari kwenda kupigana na Waajemi. Alipokuwa akingoja huko Thrasi ili apate fursa ya kuvuka mlango-bahari na kuingia Asia Ndogo, wale ‘waliokula sehemu ya chakula chake’ walitunga hila juu yake na ‘kumwangamiza.’ Alinuia kumwadhibu mwandishi wake Eros kwa sababu mambo hayakuwa shwari. Hata hivyo, Eros akaandika orodha bandia ya majina ya maofisa kadhaa waliotiwa alama wauawe. Maofisa hao walipoiona orodha hiyo walipanga njama na kumwua Aurelian.
20. “Jeshi” la mfalme wa kaskazini ‘liligharikishwaje’?
20 Mfalme wa kaskazini hakutoweka Maliki Aurelian alipokufa. Waroma wengine walitawala baada yake. Kwa muda fulani kulikuwa na maliki wa magharibi na maliki wa mashariki. Chini yao “jeshi” la mfalme wa kaskazini ‘liligharikishwa,’ au ‘kutawanywa,’b na wengi ‘walianguka wameuawa’ kwa sababu ya uvamizi wa makabila ya Kijerumani kutoka kaskazini. Wagothi walivuka mipaka ya Roma katika karne ya nne W.K. Uvamizi uliendelea, mmoja baada ya mwingine. Mwaka wa 476 W.K., kiongozi wa Ujerumani, Odoacer alimwondoa maliki wa mwisho aliyekuwa akitawala Roma. Kufikia mwanzoni mwa karne ya sita, Milki ya Roma ya upande wa magharibi ilikuwa imevunjwa-vunjwa, na wafalme Wajerumani walikuwa wakitawala Afrika Kaskazini, Gaul, Hispania, Italia, na Uingereza. Upande wa mashariki wa milki hiyo ulidumu hadi karne ya 15.
-