-
Maneno Manne Yaliyoubadili UlimwenguSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
MAANDISHI YA MKONO UKUTANI
7, 8. Karamu ya Belshaza ilikatizwaje, na hilo lilimwathirije mfalme?
7 “Saa iyo hiyo,” lasema simulizi lililopuliziwa, “vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa [“plasta,” NW] ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono ulioandika.” (Danieli 5:5) Ni jambo la ajabu kama nini! Mkono ulitokea tu, ukielea hewani karibu na sehemu yenye mwangaza mzuri ukutani. Wazia kimya kilichotokea katika karamu hiyo huku wageni walioalikwa wakizubaa na kuuangalia. Mkono huo ukaanza kuandika ujumbe wa kifumbo kwenye ukuta uliopigwa plasta.b Jambo hilo lilikuwa lenye kuashiria mabaya sana, na lisiloweza kusahaulika, hivi kwamba hata leo watu hutumia usemi “maandishi ya mkono ukutani” kuashiria hatari inayokaribia.
-
-
Maneno Manne Yaliyoubadili UlimwenguSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
b Hata jambo hilo dogo katika simulizi la Danieli limethibitika kuwa sahihi. Waakiolojia wamegundua kwamba kuta za makao ya kifalme katika Babiloni la kale zilijengwa kwa matofali na kupigwa plasta.
-