-
Aokolewa Asiliwe na Simba!Sikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
15. (a) Dario alitendaje alipopashwa habari na mawaziri na maliwali? (b) Mawaziri na maliwali walionyeshaje hata zaidi kwamba walimdharau Danieli?
15 Huenda mawaziri na maliwali walimtarajia mfalme awathawabishe kwa kazi yao ya kupeleleza kwa werevu. Ikiwa ndivyo, basi waliambulia patupu. Dario alitaabishwa sana na habari alizopashwa. Badala ya kumkasirikia Danieli au kuagiza atupwe kwenye tundu la simba mara moja, Dario alijaribu siku nzima kumwokoa. Lakini hakufua dafu.
-