-
Waovu Wataendelea Hata Lini?Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 1
-
-
15. Ni katika maana gani Yehova ‘ana macho safi hata asiweze kuangalia uovu’?
15 Hali hiyo yamsononesha sana nabii wa Yehova. Kwa hiyo, yeye asema hivi: “Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi.” (Habakuki 1:13) Naam, Yehova ‘ana macho safi hata asiweze kuangalia uovu,’ yaani, kuuvumilia ukosaji.
16. Unaweza kufafanuaje kwa ufupi mambo yaliyorekodiwa kwenye Habakuki 1:13-17?
16 Kwa hiyo, Habakuki ana maswali kadhaa yenye kuchochea fikira. Yeye auliza hivi: “Mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;
-
-
Waovu Wataendelea Hata Lini?Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 1
-
-
17. (a) Kwa kushambulia Yuda na Yerusalemu, Wababiloni wanatimizaje kusudi la Mungu? (b) Yehova atamfunulia Habakuki nini?
17 Katika kushambulia Yuda na jiji lake kuu, Yerusalemu, Wababiloni watatenda kulingana na tamaa zao wenyewe. Hawatajua kwamba wanatumiwa na Mungu kutekeleza hukumu yake ya haki dhidi ya watu wasio waaminifu. Ni rahisi kuona ni kwa nini ingekuwa vigumu kwa Habakuki kuelewa kwamba Mungu angewatumia Wababiloni waovu ili kutekeleza hukumu Yake.
-