-
“Fulizeni Kunitarajia”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
Kwa habari ya Moabu na Amoni, kulingana na Yosefo, mwanahistoria Myahudi, katika mwaka wa tano baada ya Yerusalemu kuanguka, Wababiloni walipiga vita nao na kuwashinda. Wao nao walipotelea mbali, kama ilivyotabiriwa.
-
-
“Fulizeni Kunitarajia”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
15. Yehova angeaibishaje miungu ya mataifa yaliyojitukuza juu ya watu wake?
15 Zaburi 83 hutaja mataifa kadhaa, kutia ndani Moabu, Amoni, na Ashuru, waliojitukuza juu ya Israeli, na kusema hivi kwa kujigamba: “Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, na jina la Israeli halitakumbukwa tena.” (Zaburi 83:4) Nabii Sefania alitangaza kwa moyo mkuu kwamba mataifa hayo yote yenye kiburi na miungu yayo yangeaibishwa na Yehova wa majeshi. “Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa BWANA wa majeshi, na kujitukuza juu yao. BWANA atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.”—Sefania 2:10, 11.
-
-
“Fulizeni Kunitarajia”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima.
-
-
“Fulizeni Kunitarajia”Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
14. Kuna uthibitisho gani kwamba mataifa ya kigeni ‘yalijitukuza’ juu ya Waisraeli na Mungu wao, Yehova?
14 Moabu na Amoni walikuwa maadui wa Israeli wa tangu zamani. (Linganisha Waamuzi 3:12-14.) Jiwe la Moabu, lililo katika Louvre Museum katika Paris, lina maandiko yenye taarifa ya kujisifu iliyotolewa na Mfalme Mesha wa Moabu. Yeye asimulia kwa majivuno jinsi alivyotwaa majiji kadhaa ya Israeli kwa msaada wa mungu wake Kemoshi. (2 Wafalme 1:1) Yeremia, aliyeishi wakati wa Sefania, alisema juu ya Waamoni kuwa wanakalia eneo la Israeli la Gadi katika jina la mungu wao Malkamu. (Yeremia 49:1)
-