Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
    • 6-8. Ni nini kilichotabiriwa kwenye Sefania 1:4-6, na unabii huo ulitimizwaje katika Yuda ya kale?

      6 Likitabiri matendo ya Mungu dhidi ya waabudu wasio wa kweli, andiko la Sefania 1:4-6 lasema hivi: “Nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani;

  • Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
    • 7 Mkono wa Yehova ulikuwa umenyoshwa dhidi ya watu wa Yuda na Yerusalemu. Alikuwa ameazimia kukatilia mbali katika kifo waabudu wa Baali aliyekuwa mungu wa Kanaani wa uzazi. Miungu kadhaa ya huko iliitwa Mabaali kwa kuwa walioiabudu walidhani kuwa miungu hiyo ina uvutano fulani katika mahali maalumu. Kwa mfano, kulikuwa na Baali aliyeabudiwa na Wamoabi na Wamidiani kwenye Mlima Peori. (Hesabu 25:1, 3, 6) Kotekote nchini Yuda, Yehova angewakatilia mbali makuhani wa Baali pamoja na makuhani Walawi wasio waaminifu ambao walikuwa wanakiuka sheria ya Mungu kwa kushirikiana na makuhani hao wa Baali.—Kutoka 20:2, 3.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki