-
Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
-
-
Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani.
-
-
Siku ya Hukumu ya Yehova I Karibu!Mnara wa Mlinzi—2001 | Februari 15
-
-
13. Kwa kupatana na unabii wa Sefania, ni nini ambacho kingetukia wakati Wababiloni wangeshambulia Yerusalemu?
13 “Siku ile” ambayo Yuda ilitozwa hesabu yalingana na siku ya Yehova ya kutekeleza hukumu yake dhidi ya maadui wake, kukomesha uovu, na kuthibitisha ukuu wake. Wababiloni washambuliapo Yerusalemu, kilio kingetoka katika Lango la Samaki. Huenda liliitwa hivyo kwa kuwa lilikuwa karibu na soko la samaki. (Nehemia 13:16) Magenge ya Babiloni yangeingia sehemu iitwayo mtaa wa pili, na huenda ikawa “mshindo mkuu kutoka milimani” warejezea kishindo cha Wakaldayo wanaokaribia.
-