-
Je, Mungu Hutubariki kwa Kutupa Utajiri?Amkeni!—2003 | Septemba 8
-
-
Jinsi Mungu Anavyotubariki
Yesu aliwafundisha wafuasi wake wawe na maoni yanayofaa kuhusu pesa alipowaambia ‘wakome kuhangaika’ kuhusu mali. Aliwaambia kwamba hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvaa vizuri kama mojawapo ya mayungiyungi ya kondeni. Hata hivyo, Yesu alisema: “Ikiwa Mungu huvisha hivyo mimea ya shambani, . . . je, si afadhali zaidi sana yeye atawavisha nyinyi, nyinyi wenye imani kidogo?” Yesu aliwahakikishia Wakristo kwamba ikiwa wafuasi wake wangetafuta kwanza Ufalme na uadilifu wa Mungu, basi wangeongezewa chakula, mavazi, na makao. (Mathayo 6:25, 28-33) Ahadi hiyo hutimizwaje?
Shauri la Biblia linapofuatwa, huleta baraka za kiroho. (Mithali 10:22) Hata hivyo, huleta mafanikio mengine. Kwa mfano, Neno la Mungu huwaagiza Wakristo hivi: “Mwibaji na asiibe tena, bali acheni afanye kazi ya bidii.” (Waefeso 4:28) Pia husema kwamba “Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.” (Mithali 10:4) Mara nyingi waajiri hupenda Wakristo wanyofu, wenye bidii wanaofuata shauri hilo. Hilo laweza kuwa baraka.
Pia, Biblia huwafundisha Wakristo waepuke kuwa na pupa kwa kucheza kamari, zoea chafu la kuvuta sigara, na zoea lenye kudhuru la kulewa. (1 Wakorintho 6:9, 10; 2 Wakorintho 7:1; Waefeso 5:5) Wanaofuata shauri hili hupunguza gharama zao na afya zao huwa bora zaidi.
-
-
Je, Mungu Hutubariki kwa Kutupa Utajiri?Amkeni!—2003 | Septemba 8
-
-
Yehova Mungu huwabariki wale wanaojitahidi kufanya mapenzi yake. (Zaburi 1:2, 3) Yeye huwapa nguvu na uwezo wa kukabiliana na majaribu, kuruzuku familia zao, na kuutafuta kwanza Ufalme wake. (Zaburi 37:25; Mathayo 6:31-33; Wafilipi 4:12, 13)
-