-
Alikuwa Mshikamanifu Alipokabili MajaribuMnara wa Mlinzi—2010 | Januari 1
-
-
Adumisha Ushikamanifu Anaporekebishwa
Muda mfupi baada ya wakati huo wenye shughuli nyingi, Yesu aliongoza mitume wake na baadhi ya wanafunzi wake, katika safari ndefu kuelekea kaskazini. Nyakati nyingine, kilele chenye theluji cha Mlima Hermoni, uliokuwa upande wa kaskazini zaidi mwa Nchi ya Ahadi, kilionekana kutoka kwenye Bahari ya Galilaya yenye maji ya bluu. Hatua kwa hatua, sehemu kubwa ya mlima huo ilionekana kadiri walivyoukaribia, wakipanda eneo lenye mwinuko kuelekea kwenye vijiji fulani karibu na Kaisaria Filipi.c Wakiwa katika mandhari hii yenye kuvutia, ambapo wangeweza kuona sehemu kubwa ya Nchi ya Ahadi upande wa kusini, Yesu aliwauliza wafuasi wake swali fulani muhimu.
Aliwauliza hivi: “Umati unasema mimi ni nani?” Tunaweza kuwazia Petro akiyatazama macho ya Yesu yenye utambuzi, na kwa mara nyingine akatambua jinsi Bwana wake alivyokuwa mwenye fadhili na akili nyingi. Yesu alitaka kujua maoni ya wasikilizaji wake kuhusu mambo waliyoona na kusikia.
-
-
Alikuwa Mshikamanifu Alipokabili MajaribuMnara wa Mlinzi—2010 | Januari 1
-
-
c Katika safari yao ya kilomita 48, Yesu pamoja na wale walioandamana naye walipanda kutoka fuo za Bahari ya Galilaya, ambazo ziko mita 210 hivi chini ya usawa wa bahari na kufika eneo lililo mita 350 hivi juu ya usawa wa bahari. Walipita katika maeneo yenye kuvutia sana.
-