Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Ajapo Katika Utukufu wa Ufalme
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
    • 3, 4. (a) Yesu alisema nini siku sita kabla ya mgeuko-umbo? (b) Fafanua yale yaliyotukia wakati wa mgeuko-umbo.

      3 Siku sita kabla ya mgeuko-umbo, Yesu aliwaambia wafuasi wake hivi: “Mwana wa binadamu akusudiwa kuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, na ndipo atakapomlipa kila mmoja kulingana na mwenendo wake.” Maneno hayo yangetimizwa kwenye “umalizio wa mfumo wa mambo.” Yesu aliendelea kutaarifu hivi: “Kwa kweli nawaambia nyinyi kwamba kuna baadhi ya wale ambao wamesimama hapa ambao hawataonja kifo hata kidogo mpaka kwanza wamwone Mwana wa binadamu akija katika ufalme wake.” (Mathayo 16:27, 28; 24:3; 25:31-34, 41; Danieli 12:4) Mgeuko-umbo ulitukia ukiwa utimizo wa maneno hayo ya mwisho.

  • Yesu Ajapo Katika Utukufu wa Ufalme
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 15
    • 5. Mgeuko-umbo ulimwathirije mtume Petro?

      5 Mtume Petro tayari alikuwa amemtambua Yesu kuwa “Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” (Mathayo 16:16) Maneno ya Yehova kutoka mbinguni yalithibitisha utambulisho huo, na ono la kugeuka umbo kwa Yesu lilikuwa mwonjo wa kimbele wa kuja kwa Kristo katika nguvu na utukufu wa Ufalme, kuwahukumu wanadamu hatimaye. Miaka zaidi ya 30 baada ya mgeuko-umbo, Petro aliandika hivi: “Haikuwa kwa kufuata hadithi zisizo za kweli zilizotungwa kwa usanifu mwingi kwamba tuliwafahamisha nyinyi juu ya nguvu na kuwapo kwa Bwana wetu Yesu Kristo, lakini ilikuwa kwa kupata kuwa mashahidi wa kujionea fahari yake. Kwa maana alipokea kutoka kwa Mungu Baba heshima na utukufu, wakati maneno ya namna hii yalipopelekwa kwake kwa utukufu wenye fahari: ‘Huyu ni mwana wangu, mpendwa wangu, ambaye mimi mwenyewe nimemkubali.’ Ndiyo, maneno haya tuliyasikia yakipelekwa kutoka mbinguni tulipokuwa tungali pamoja naye katika mlima mtakatifu.”—2 Petro 1:16-18; 1 Petro 4:17.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki