Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kile Kinachohitajiwa Hasa ili Kuwa na Furaha
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Septemba 1
    • Hata hivyo, huenda tukashangaa jinsi watu walio na njaa na walio na kiu kwa ajili ya uadilifu au wanaoomboleza wanavyoweza kutajwa kuwa wenye furaha. Watu hao huona hali za ulimwengu jinsi zilivyo kikweli. Wao ‘huugua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanywa’ siku zetu. (Ezekieli 9:4) Kuugua na kulia hakuwaletei furaha. Hata hivyo, wanapojifunza kuhusu kusudi la Mungu la kuwapa haki waliokandamizwa na kuleta hali za uadilifu duniani, wanafurahi sana.—Isaya 11:4.

  • Kile Kinachohitajiwa Hasa ili Kuwa na Furaha
    Mnara wa Mlinzi—2004 | Septemba 1
    • Watu wanaoomboleza, walio na njaa na kiu ya uadilifu, na wanaotambua uhitaji wao wa kiroho hufahamu umuhimu wa kuwa na uhusiano mzuri pamoja na Muumba. Kuwa na uhusiano mzuri pamoja na watu huleta furaha, lakini kuwa na uhusiano mzuri pamoja na Mungu huleta furaha kubwa hata zaidi. Naam, hapana shaka kwamba wale ambao kwa kweli wanapenda yaliyo sawa, na ambao wako tayari kukubali mwongozo wa Mungu, wanaweza kutajwa kuwa wenye furaha ya kweli.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki