Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jinsi Unavyoweza Kupata Mafanikio ya Kweli Maishani
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Desemba 15
    • 13. Yesu alitoa shauri gani kuhusu kujiwekea hazina?

      13 Yesu alisema hivi kuhusu hazina: “Acheni kujiwekea hazina duniani, ambako nondo na kutu hula, na ambako wezi huvunja na kuiba.

  • Jinsi Unavyoweza Kupata Mafanikio ya Kweli Maishani
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Desemba 15
    • Kwa maana mahali ilipo hazina yako, ndipo moyo wako utakapokuwa pia.”—Mt. 6:19-21.

  • Jinsi Unavyoweza Kupata Mafanikio ya Kweli Maishani
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Desemba 15
    • 14. Kwa nini si hekima kutafuta hazina za ulimwengu?

      14 Hazina ambazo mtu anaweza kujiwekea duniani zinaweza kuwa zaidi ya pesa tu. Kwa njia fulani, zinaweza kutia ndani chochote kati ya vitu ambavyo Sulemani aliandika kuvihusu vinavyoonwa na watu kuwa kipimo cha mafanikio, yaani, sifa, umashuhuri, au mamlaka. Yesu alikazia jambo lilelile ambalo Sulemani alikazia katika kitabu cha Mhubiri—hazina za ulimwengu hazidumu. Kama vile tu ambavyo huenda umejionea katika ulimwengu unaokuzunguka, hazina hizo zote zinaweza kuharibika na kupotea kwa urahisi. Profesa F. Dale Bruner aliandika hivi kuhusu hazina za aina hiyo: “Inajulikana wazi kwamba umashuhuri haudumu. Mtu aliye mashuhuri leo anasahauliwa kesho. Mtu aliye na pesa nyingi mwaka huu huenda akafilisika mwaka ujao. . . . [Yesu] anawapenda wanadamu. Anawasaidia kuepuka kutamauka ambako bila shaka kunasababishwa na utukufu ambao haudumu, unaotoweka upesi. Yesu hataki wanafunzi [wake] watamauke. ‘Kila siku, ulimwengu humgeuzia kisogo mtu fulani ambaye alikuwa maarufu sana.’” Ingawa watu wengi huenda wakakubali maneno hayo, ni wangapi wanaoruhusu maneno hayo ya hakika yabadili njia yao ya maisha?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki