-
“Mwacheni Msomaji Atumie Ufahamu”Mnara wa Mlinzi—1999 | Mei 1
-
-
Mwacheni mtu aliye juu ya paa ya nyumba asiteremke, wala asiingie ndani kuchukua kitu chochote kutoka nyumbani mwake; na mwacheni mtu aliye katika shamba asirudi kwa mambo yaliyo nyuma kuchukua vazi lake la nje.
-
-
“Mwacheni Msomaji Atumie Ufahamu”Mnara wa Mlinzi—1999 | Mei 1
-
-
Pia, ni jambo lenye maana kwamba Yesu alionya kuhusu mtu kurudi nyumbani mwake ili kuchukua nguo na bidhaa nyingine. (Mathayo 24:17, 18) Kwa hiyo, huenda majaribu yako mbele kuhusiana na jinsi tunavyoziona mali za kimwili; je, hivyo ndivyo vitu muhimu zaidi, au je, ule wokovu utakaowajia wale wote walio upande wa Mungu ni wa muhimu zaidi? Naam, huenda kukimbia kwetu kukahusisha magumu fulani na hasara. Itatubidi tuwe tayari kufanya lolote lihitajiwalo, kama walivyofanya Wakristo wenzetu wa karne ya kwanza, ambao walikimbia kutoka Yudea hadi Perea, iliyo ng’ambo ya Yordani.
-