Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Januari 1
    • Ni bamba la aina gani la kuandikia linalotajwa katika Luka 1:63?

      ▪ Injili ya Luka inataja kwamba marafiki wa Zekaria walimuuliza kuhusu jina la mwana wake aliyekuwa amezaliwa majuzi. Zekaria “akaomba bamba na kuandika: ‘Yohana ndilo jina lake.’” (Luka 1:63) Kulingana na kitabu kimoja cha wataalamu, neno la Kigiriki linalotafsiriwa “bamba” katika andiko hilo linamaanisha “bamba dogo la mbao la kuandikia, lililopakwa nta kwenye sehemu ya juu.” Mabamba ya mbao yaliyokuwa yameunganishwa pamoja, yalipakwa nta laini ya nyuki. Mwandikaji aliandika kwenye mabamba hayo kwa kutumia kifaa fulani kilichochongoka. Baadaye maandishi yalifutwa na yale mabamba yaliweza kutumiwa tena.

      Kitabu kimoja kuhusu kusoma na kuandika wakati wa Yesu (Reading and Writing in the Time of Jesus) kinasema hivi: “Michoro ambayo imepatikana Pompeii, na sanamu kutoka sehemu mbalimbali za Milki ya Roma, zinaonyesha kwamba mabamba kama hayo yalitumiwa kwa ukawaida. Yamechimbuliwa pia katika sehemu nyingi, kuanzia Misri hadi Ukuta wa Hadriani [Uingereza Kaskazini].” Yaelekea, watu kama vile wanabiashara, maofisa wa serikali, na labda hata baadhi ya Wakristo wa karne ya kwanza, walitumia mabamba kama hayo.

  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Januari 1
    • [Picha katika ukurasa wa 11]

      Bamba la nta la mtoto wa shule, miaka ya 100 W.K.

      [Hisani]

      By permission of the British Library

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki