Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • Hata alienda na kujiambatanisha mwenyewe kwa mmoja wa raia wa nchi hiyo, naye akamtuma aingie katika mashamba yake ili achunge mifugo ya nguruwe.

  • “Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • Luka 15:14-16

  • “Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • Badala yake, alifahamiana na raia fulani aliyemwajiri kazi ya kuchunga nguruwe. Kwa kuwa Sheria ya Kimusa ilisema kwamba nguruwe walikuwa wanyama wasio safi, yaelekea Myahudi hangekubali kazi kama hiyo. (Mambo ya Walawi 11:7, 8) Lakini ikiwa dhamiri ya mwana mpotevu ilimsumbua, ilimbidi aizime. Kwa vyovyote, hangeweza kumtarajia mwajiri wake, raia wa mahali hapo, ahangaishwe na hisia za mtoka-ugenini aliye fukara. Hali hiyo mbaya ya mwana mpotevu iko sawa na ile inayowapata watu wengi leo ambao huacha njia iliyonyoka ya ibada safi. Mara nyingi, watu hao hujishughulisha na mambo ambayo hapo awali wangeyafikiria kuwa yenye kushusha. Kwa kielelezo, akiwa na umri wa miaka 17, mwanamume mmoja kijana alikaidi malezi yake ya Kikristo. “Kukosa maadili na matumizi mabaya ya dawa za kulevya yalibatilisha miaka mingi ya mafundisho yaliyotegemea Biblia,” yeye akubali. Punde si punde, mwanamume huyo kijana alijipata gerezani kwa sababu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na uuaji kimakusudi. Ingawa baadaye alipata nguvu tena kiroho, alipatwa na mateso makubwa kama nini kwa sababu ya “mfurahio wa muda wa dhambi”!—Linganisha Waebrania 11:24-26.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki